top of page
landscape-1520344613-gettyimages-517003864.jpg

Lugha za Nairobi

Languages of Nairobi 

Lugha za Nairoibi is a long-term collaborative research project between Washington University and the University of Nairobi, dedicated to documenting, mapping, and analyzing the complex linguistic profile of Nairobi, Kenya. This project seeks to bring greater visibility to patterns of language contact and migration-driven multilingualism that shape the linguistic landscape in Africa's rapidly growing cities.

The Project: Vision, Origins and Methodology

Lugha za Nairobi was launched in 2020 through the Carnegie African Diaspora Fellowship Program. The 2020 and 2021 fellowship awards enabled Professor Mungai Muntonya and Professor Iribe Mwangi to co-design a scalable research framework for documenting the multilingual patterns of Nairobi. The guiding objective is to produce language distribution maps that reflect contact and distribution patterns of Kenyan and African immigrant languages in the densely multilingual city and beyond. Hopefully, the project inspires further research in other urban centers across the continent. 

On this website, you will find:

  • Interactive maps showing dominant Kenyan languages across Nairobi's subcounties and neighborhoods

  • Data visualizations and statistics on migration patterns, language use, and community demographics within Nairobi.

  • Background information on Nairobi's multilingual urban history, including themes of migration, resettlement, and language contact.

 

The Lugha za Nairobi project stands as a model for urban linguistic research in Africa, highlighting the importance of documenting and understanding the complexities of language use in rapidly changing urban environments. We look forward to collaboration with researchers interested in launching similar language mapping projects in other African metropolises. 

The English version of this Swahili website will be available soon

About Lugha za Nairobi
 

Ramani zifuatazo zinaonyesha lugha tatukuu zinazosemwa kila kaunti ndogo. Ramani ya upande wa kushoto ni ya lugha asili za Kenya ilhali ya kulia ni ya lugha zisemazwo na Waafrika waliohamia Nairobi. Data tuliyoitumia kuwasilisha ramani hizi mbili inapakitana katika matokeo rasmi ya hesabu ya watu (sensa) ya kitaifa ya 2019. Ingawa shughuli ya ukusanyanji data ya sensa haiwaulizi washiriki lugha wazisemazo, kabila zao hutambuliwa. Tumehusisha lugha na kabila katika mchakato wa uchoraji ramni hizi tukilelewa bayana kuwa siyo kila mzawa wa kabila fulani husema lugha mama.  Aidha, yetu ni hatua moja inayotuhimiza sote tuchangie kuliziba pengo la ukosefu wa data kuhusu lugha za Kiafrika jijini Nairobi na kwingineko Afrika kama alivyotuhimiza shujaa na msomi tajika, mwendazake Profesa Ngugi wa Thiong'o.

Lugha za Kikenya
Kenyan Languages

Lugha za Kwingineko

Screen Shot 2024-11-19 at 7.52.07 PM.png
Screen Shot 2024-11-19 at 8.00_edited.jpg

Nairobi Language Map Project
Mutonya & Iribe

Nairobi Language Map Project
Mutonya & Iribe

Usambazaji wa Lugha Nairobi
 

Language Distribution in Nairobi

Screen Shot 2024-11-19 at 7.47.17 PM.png

Add a Title

Lugha za Nairobi: Muktadha

Heading 2

Languages in Context

Lugha za Kikenya

Kwa mujibu wa Sensa ya Kenya 2019 lugha na lahaja nyingi za Kikenya zinasemwa katika sehemu mbalimbali za mitaa na vitongoji 

Tarakwimu za Sensa 2019 pamoja na utafiti wetu zinaonyesha raia wengi wa mataifa ya kanda za mashariki, kati, na kusini mwa Afrika wamehamia Nairobi. Lugha zao zinasikika katika sehemu anuwai za Nairobi. 

Lugha za Kigeni: Kongwe

Lugha za Kiarabu, Kihindi, Kiajemi, Kigujarati, Kiingereza, na nyinginezo zina historia ndefu jijini Nairobi

Lugha za Kigeni: Mpya

Lugha ambazo zimenata makini ya Wanairobi hivi karibuni ni pamoja na Kichina, Kihispania

Mtagusano wa Lugha

Kabla ya ujenzi wa jiji la Nairobi, eneo hili lilishuhudia maingiliano ya lugha kutoka  kwa wasafiri, wafanyabiashara, wawindaji, wamisheni, na wengi kutoka maeneo tofauti dunia: Afrika, Ulaya, Esia, n.k. Lugha zao ziliingiliana na kuathiriana na za wenyeji.

Screen Shot 2024-11-19 at 7.37.19 PM.png

Wenyeji wa Nairobi: Maoni Kuhusu Lugha
Nairobians: Mental Maps
 

Screen Shot 2024-11-26 at 2.57.54 PM.png

Wanafunzi sitini na wawili wa darasa la Dkt. Basilio Mung'ania (Chuo Kikuu cha Nairobi, mwaka 2021) walishiriki utafiti wa kiisimujamii wa kubaini utambuzi wao wa lugha katika kaunti ya Nairobi. Matokeo yamewasilishwa kwenye mraba yaonyesha jinsi wanafunzi hao walivyoidhania ramani la lugha ya Nairobi. Kwa maoni yao, lugha nane kuu za Kenya "husikika kwa wingi" na "kwa uzito tofauti" katika kaunti ya Nairobi. Kwa kifupi mraba unaonyesha wanafunzi wanaamini zaidi ya asilimia 85% ya wakazi wa Kibra, Eastleigh, na Githurai husema lugha moja: Kijaluo, Kisomali, na Kikikuyu mtawalia. Kwingineko lugha kuu mbili, tatu, na nne zinasikika kwa wingi kukiwepo na lugha mbili kuu zinazoshindana.

Matokeo ya Sensa 2019

Screen Shot 2024-11-26 at 3.01.13 PM.png

Namba za Nairobi

Nairobi by
the
Numbers

17

Kaunti ya Nairobi imegawanywa kuwa na kaunti ndogo 17.  Sensa ya mwaka 2019 ilikadiria idadi ya wakazi wa kaunti ya Nairobi kuwa takribani milioni nne nukta tatu. Lakini ripoti za 2024 zinakadiria idadi hiyo kuongezeka hata milioni sita hivi.

Mwaka 1899 eneo lililojulikana kwa lugha ya Kimaa kama "Enkare Nyrobi" likatwaliwa kuwa makao makuu ya reli ya kikoloni iliyotoka Mombasa hadi Kampala. Jiji la Nairobi lina umri wa miaka 126

126
47

Mwaka 2010 katiba iligatua utawala nchini Kenya kuwa kaunti 47.  Licha ya ubabe na umaarufu wake kaunti ya Nairobi iliorodheshwa  namba ya mwisho (47) badala ya kwanza (1).

70

Jumla ya lugha zisemwazo Nairobi zinazidi 70 zikiwemo za Kikenya, za lugha anuwai kutoka  mataifa mengi barani Afrika, na kwingineko duniani.

Namba za Nairobi

Nairobi by the Numbers 

My Projects

Kaunti ya Nairobi imegawanywa kuwa na kaunti ndogo 17.  Sensa ya mwaka 2019 ilikadiria idadi ya wakazi wa kaunti ya Nairobi kuwa takribani milioni nne nukta tatu. Lakini ripoti za 2024 zinakadiria idadi hiyo kuongezeka hata milioni sita hivi.

17

Mwaka 1899 eneo lililojulikana kwa lugha ya Kimaa kama "Enkare Nyrobi" likatwaliwa kuwa makao makuu ya reli ya kikoloni iliyotoka Mombasa hadi Kampala. Jiji la Nairobi lina umri wa miaka 124

124

3

Mwaka 2010 katiba iligatua utawala nchini Kenya kuwa kaunti 47.  Licha ya ubabe na umaarufu wake kaunti ya Nairobi iliorodheshwa  namba ya mwisho (47) badala ya kwanza (1).

17

2

Jumla ya lugha zisemwazo Nairobi zinazidi 70 zikiwemo za Kikenya, za lugha anuwai kutoka  mataifa mengi barani Afrika, na kwingineko duniani.

70

4

Jiografia ya Lugha ya Nairobi
 

Screen Shot 2024-11-27 at 6.06.54 PM.png

Nairobi ni jiji kuu na makao makuu ya serikali ya Kenya na mashirika mengi ya kimataifa. Jiji la Nairobi linapatikana eneo la kati nchini Kenya baina ya pwani ya Bahari ya Hindi na ukingo wa Ziwa Nyanza. Kaunti ya Nairobi imepakana na kaunti za Kiambu, Machakos, na Kajiado. Kaunti hizi jirani zina asilimia kubwa ya wasemaji lugha za Kikuyu, Kikamba, na Kimaa, mtawalia. Nairobi ina utajiri mkubwa sana wa lugha anuwai kutoka pembe zote za Kenya, Afrika, na dunia.


Baada ya Kenya kujinyakulia uhuru wananchi waliohamia jiji kutoka mashinani wamekuwa wakichagua kuishi mitaa fulani kutoka na sababu anuai kama vile upatikanaji kazi, gharama ya maisha, elimu, aila na lugha za wakazi wa mtaa huo, na kadhalika. Ramani hii inaonyesha lugha tatu kuu zinazosemwa na wakazi wa kila kaunti ndogo ya Nairobi. Utafiti unaendelea na tutabainisha vyema zaidi mgawanyo huu wa lugha.

Screen Shot 2024-11-27 at 6.06.54 PM.png

Jiografia ya Lugha ya Nairobi
 

Nairobi ni jiji kuu na makao makuu ya serikali ya Kenya na mashirika mengi ya kimataifa. Jiji la Nairobi linapatikana eneo la kati nchini Kenya baina ya pwani ya Bahari ya Hindi na ukingo wa Ziwa Nyanza. Kaunti ya Nairobi imepakana na kaunti za Kiambu, Machakos, na Kajiado. Kaunti hizi jirani zina asilimia kubwa ya wasemaji lugha za Kikuyu, Kikamba, na Kimaa, mtawalia. Nairobi ina utajiri mkubwa sana wa lugha anuwai kutoka pembe zote za Kenya, Afrika, na dunia.


Baada ya Kenya kujinyakulia uhuru wananchi waliohamia jiji kutoka mashinani wamekuwa wakichagua kuishi mitaa fulani kutoka na sababu anuai kama vile upatikanaji kazi, gharama ya maisha, elimu, aila na lugha za wakazi wa mtaa huo, na kadhalika. Ramani hii inaonyesha lugha tatu kuu zinazosemwa na wakazi wa kila kaunti ndogo ya Nairobi. Utafiti unaendelea na tutabainisha vyema zaidi mgawanyo huu wa lugha.

Screen Shot 2024-11-19 at 10.03.06 PM.png

Karasani

Screen Shot 2024-11-19 at 10.04.05 PM.png

Mitaa: Neighbourhoods

Parklands

Screen Shot 2024-11-19 at 10.03.48 PM.png

Westlands

Screen Shot 2024-11-19 at 10.21.05 PM.png

Embakasi

Screen Shot 2024-11-19 at 10.03.28 PM.png

Njiru

Nijuru

Lugha za Waafrika Waliohamia Nairobi
Immigrant Languages

Awamu ya kwanza ya mradi huu inashughulikia wasemaji lugha waliotoka nchi lengwa za Barani Afrika. Haya ni makundi ya wanalugha ambayo hayajaangaziwa kiutafiti na mradi unakusudia kuchangia mkabala unaochanganya isimujamii na taaluma nyinginezo.

Kutokana na ramani hii ni dhahiri kwamba kuna wahamiaji kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika wanaoishi pamoja na Wakenya jijini Nairobi. Jumuiya za wasemaji lugha kutoka nchi jirani za Kenya (Uganda, Tanzania, Somalia, Sudan Kusini, na Ethiopia) ni 74% ya idadi ya Waafrika waliohamia Nairobi. Aidha, jumuiya za watu kutoka DR Kongo, Kongo, Burundi na Rwanda ni asilimia 22%; Nigeria na Eritrea ni 1.4%, huku wale kutoka kusini mwa Afrika (Afrika Kusini, Zambia, na Zimbabwe) ni 1.6%.

Bonyeza nchi zilizoangaziwa kwenye ramani ili usome taarifa zaidi. (Ryan Sears, Audrey Nickels, na Profesa Mutonya walishirikiana kuiunda ramani hii darasani). 

Screen Shot 2024-11-27 at 6.12.21 PM.png

Lugha Kutoka Kwingineko Afrika

Lugha kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika zinasikika katika maeneo mengi ya kaunti ya Nairobi. Lugha 3 kuu kutoka kwingineko Afrika na zinazosemwa katika kaunti ndogo tofauti za Nairobi zimeorodheshwa katika jedwali hili. Asilimia zilizomo zinaashiria idadi ya wanajumuiya hao ikilinganishwa na jumla ya Waafrika wahamaji wote katika kaunti ndogo hiyo. Kwa mfano, katika kaunti ndogo ya Kamukunji lugha za Kisomali ni asilimia 56, za kutoka Uhabeshi ni asilimia 14, nazo za Uganda ni asimilia 13 ya lugha zote za Waafrika wahamaji wanaoishi Kamukunji. Uchambuzi zaidi unapatikana katika sehemu ya 'Ramani za Nairobi' ya tovuti hii.

Screen Shot 2024-11-19 at 10.40.50 PM.png

Idadi kubwa ya wahamiaji kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika inaashiria hadhi ya Nairobi barani Afrika. Lugha za wahamaji hao Waafrika zinapoingiliana na lugha za Kikenya mitaani, sokoni, michezoni, shuleni, na katika shamrashamra nyinginezo, zinaathiriana na kubadilishana. Mtagusano huu wa lugha hauna budi kuongeza hulka ya kiisimu ya Nairobi na kuchangia mabadiliko ya lugha za Kiswahili, Sheng, na lugha nyinginezo. 

Wakuu wa Mradi: Mutonya na Iribe

Screen Shot 2023-07-24 at 1_36_edited_jp.webp
3d2037_0c83b1868362474692b6b84d37c0e647~mv2.webp

Kuhusu Mradi Huu
About this  Project

Mradi huu uliasisiwa mwaka 2020 chini ya ufadhili wa Carnegie African Diaspora Fellowship Program (CADFP). Tuzo ya CADFP ilimwezesha Profesa Mungai Mutonya wa Chuo Kikuu cha Washington University Mjini St. Louis na mwana-CADFP mwenzake, Profesa Iribe Mwangi, aliye Mwenyekiti wa Idara ya Kiswahili, Chuo Kikuu cha Nairobi (UoN), kubuni mikakati mwafaka ya kiutafiti inayoendeleza mradi hadi sasa. Tuzo ya CADFP 2022 iliongezea ushirikiano wa kiutafiti na kuwezesha mradi kupiga hatua muhimu.  Lengo kuu la mradi huu ni kusawiri kwa njia ya ramani, mtagusano changamana wa lugha unaotokana na uhamiaji kutoka nchi mbalimbali za Afrika. Aidha, mradi unaangazia hali changamana ya lugha jijini Nairobi na uhalisi wa kimawasiliano katika jiji hili kuu la Afrika Mashariki.Tovuti hii inalenga jumuiya zifuatazo:

Wenyeji wa Nairobi wanaopenda kuyafahamu mazingira yao

Wenyeji waliohamia Nairobi kutoka nchi mbalimbali na waliokubali kuhojiwa

Wenyeji wa Nairobi walio na ukarimu wa kuwakaribisha na kuishi kwa amani na wenyeji wapya walio na lugha na asili tofauti.-

Wenyeji kutoka sehemu mbalimbali za Kenya, Afrika, waliohamia Nairobi  kusoma na kujitafutia riziki.

Mradi huu unatambua mchango wasomi, watafiti, walimu, wanafunzi, waandishi habari, na wote wanaoangazia masiala ya matumizi ya lugha jijini Nairobi.  

Washirika Wakuu
Mradi huu haungewezekana pasingekuwepo na hisani ya watu wengi na mashirika yaliyotajwa hapa chini. Watafiti wasaidizi, wahojiwa, wanafunzi wetu na wasomi wenzetu idarani, na, hususan, Mtiva Ephrahim Wahome. Sifa za mradi huu zihusishwe nao; dosari zozote ni zetu wasimamizi wa mradi.

Screen Shot 2024-11-27 at 6.33.40 PM.png
Screen Shot 2024-11-27 at 6.32.01 PM.png
Screen Shot 2024-11-27 at 6.23.32 PM.png
Screen Shot 2024-11-27 at 6.35.06 PM.png
Screen Shot 2024-11-27 at 6.36.50 PM.png
Screen Shot 2024-11-27 at 6.36.13 PM.png
Screen Shot 2024-11-27 at 6.29.14 PM.png
bottom of page