top of page
Screen Shot 2025-11-04 at 1.57.24 PM.png

Enkare Nyrobi

Jina asili la Nairobi ni Enkare Nyrobi (yaani eneo lenye maji baridi). Ni jina linalotoka lugha ya wenyeji asili wa eneo hilo: Wamasai.

Mwaka 1899 kampuni ya kikoloni iliyopewa kandarasi ya ujenzi wa reli kutoka Mombasa hadi Kampala ilihamisha makao yake makuu kutoka Masaku hadi eneo lililojulikana kama Enkare Nyrobi.

Kabla mwaka 1899 eneo lijulikanalo sasa kama jiji la Nairobi lilikuwa eneo lenye masoko na kambi ya kuwafariji wanamisafara. Misafara ilikuwa na malengo tofauti na iliwajumuisha wanabiashara, wawindaji, wamisheni, na wazungu waliotumwa na nchi za Ulaya kupata habari za Afrika. Misafara iliyoanza Mombasa ilipiga guu kwa majuma na miezi kabla ya kufikia sehemu hii ya katikati mwa nchi ya Kenya.

Kama ramani iliyoko hapo chini ya takriban mwaka 1898 inavyodhihirisha kati ya nchi za Wamasai na Wakikuyu na maeneo sambamba na mito ya Gitathuru, Mathare, na Nairobi yaliwapatia wasafiri waliotumia barabara ya Sclater huduma muhimu kama malazi na chakula. Soko la Dagoretti lilikuwa miongoni mwa masoko muhimu kwa wanamisafara. 

Historia ya
Nairobi

Mji Mpya

Reli ilipofika Nairobi mwaka 1899, wakazi wapya na wa kwanza wakawa ni wafanyakazi na maofisa wa reli. Kama picha hii inavyoonyesha miundomsingi ilikwa sahili, ila ilikuwa kwa kasi sana.

Kutoka mwaka 1899 hadi 1905, taswira na hulka ya mji mkubwa wa kwanza kuibuka - ambao haukuwa wa kipwani kama vile miji ya Lamu, Malindi, na Mombasa - ilijitokeza. Mji huu wa bara ulikua kwa haraka sana kukidhi mahitaji anuai ya wakazi wapya waliokuwa na maslahi kinzani. Wahamaji kutoka sehemu za nyingi za nchi ya Kenya na kwingineko walichangia ukarabati wa miundomsingi na mahitaji anuai ya mji.

Ramani ya mwaka 1903 (pia kwa hisani ya McVicar 1968) inadhihirisha mambo matatu muhimu. Kwanza, reli ilikuwa kichocheo kikuu cha ukuaji wa mji, hususan miaka ya uchanga wa Nairobi. Pili, shughuli za uendelezaji wa ghala la reli na kituo cha garimoshi zilichangia upanuzi wa serikali (Govt. Offices) jeshi (B.E.A Rifles), mitaa (Lower Level Railway Housing (Muthurwa) na Government Officers' Houses (Upper Hill)), na biashara (Indian Bazaar, African Market). Hata hivyo, shughuli za reli zilichangia hulka ya ubaguzi wa rangi na kiuchumi ambao bado unadhihirika katika mpangilio wa mji na mitaa ya Nairobi. Haswa, ramani inaonyesha maeneo yaliyotengewa Waafrika, Wazungu, na Wahindi. Vilevile kuna mitaa ya wafanyikazi wa viwango vya chini, kati, na juu. Tatu, ni dhahiri kuwa wakazi watangulizi wa Nairobi walisema lugha tofauti kutoka Kenya na Afrika, Esia, na Ulaya, Kiafrika. Bila shaka mji ulikuwa na hulka ya uwingilugha. Ingawa mfumo wa kikoloni uliendeleza sera zilizotenganisha makundi ya wakazi kufuatia msingi ya kirangi, kikabila, na kiuchumi hali haijabadilika sana tangu Kenya ilipojinyakulia uhuru mwaka wa 1963. Mradi huu umebaini mgawanyiko wa kiisimu, kikabila, na hata kitaifa unaendelea pindi jiji linavyokua na kuwapata wakazi wapya. 

Ramani zilizorejelea hapo juu za eneo la Nairobi kabla ya ujenzi wa reli (takriban mwaka 1898), na mji ulivyokuwa miaka mitano baadaye (1903). Ramani zote mbili kwa hisani ya McVicar, 1968).

Screen Shot 2025-11-04 at 1.57.24 PM.png

Enkare Nyrobi

Mwaka 2010 katiba mpya ya Kenya iliigawanya nchi kuwa kaunti 47.

  • Nairobi ni kaunti namba 047.

    • Ina idadi ya wakazi 4,397,073 

    • Imegawanywa zaidi kwa kaunti ndogo 17

    • Dagoretti, Embakasi, Kamukunji, Kasarani, Kibra, Langata, Makadara, Mathare,  Ruaraka​   Roysambu  Starehe, Westlands

​

Kaunti Ndogo
za Nairobi

Screen Shot 2024-11-20 at 11.34.39 AM.png
Screen Shot 2025-11-04 at 1.57.24 PM.png

Lugha zisemazwo Nairobi

Screen Shot 2024-11-20 at 11.48.00 AM.png

Lugha za Kikenya

Kikuyu, Kiluhya (Kibukusu, Kimaragoli, Kisamia, n.k.), Kidholuo, Kikamba, Kisomali, Kikisii, Kimeru, Kigiriama, Kimaasai, Kinandi, Kikipsigis, Kioromo, n.k.

Lugha za Kutoka Kwingineko AfrikaLugha kutoka Uganda (Kiganda, Kinyankole, Ethiopia, Rwanda, Burundi, Kongo, Zambia, Zimbabwe, Afrika Kusini, Sudan Kusini, n.k.

Miongoni mwa lugha kuu zinazosemwa Nairobi ni pamoja na kutoka Kenya, mataifa mengine ya Afrika, Uarabuni, Esia, Ulaya, Amerika, na kwingineko.

Screen Shot 2024-11-20 at 10.51.20 AM.png

Khoja Mosque 

Screen Shot 2024-11-20 at 10.51.48 AM.png
Screen Shot 2024-11-20 at 10.52.08 AM.png

Mbali na michezo, kituo cha Baptist Center iliwapa vijana chumba au darasa la kufanya “Homework” wakati wa jioni kwa sababu nyumba nyingi hapo Eastlando hazikuwa na umeme. Baadhi ya wachezaji mashuhuri kutoka Kaloleni ni Nick Akura, Peter Pierre Ochieng, George “Vigo” Otieno, Jerry Imbo, Edward Kiiza, Neville Pudo, Joe Oyando, John Busolo, Lumumba Magunga, Jeff Fwaya, Jomo Opwande, na Mark Shida. Black Mamba Sports club pia ilikuwa na timu hodari sana ya Handball

Vijana wa Black Mamba na Kaloleni Welfare walizungumza lugha ya Sheng kwa sababu walitoka katika jamii mbali mbali za Kenya na pia Uganda (kwa mfano Edward Kizza na nduguze ambo walikuwa wachezaji hodari wa kandanda).

Hapo katika uga wa Majimbo ulioko mtaa wa Kaloleni, kulikuwa na mashindano ya mpira, kila mwaka wakati wa likizo ya Aprili, ulio julikana kama “Majimbo Tournament.” Haya mashindano ya majimbo yalikuwa yanajumuisha majimbo ya mkoa wa Luo Nyanza (nadhani hii ndiyo ilikuwa asili ya jina la huo uga - Majimbo Field). Majimbo haya yalikuwa kama Alego, Ugenya, Imbo, Sakwa, Uyoma, na mengine ya South Nyanza. Washiriki wa mashindano ya Majimbo walikuwa wakitoka katika sehemu zote za Nairobi, sio tu wakaazi wa Kaloleni.

Lugha ulizozisisikia zikisemwa Nairobi mitaani, shuleni, viwanjani, na kwingineko ulipokuwa mdogo. Nilipokuwa mdogo, lugha ambazo nilizisikia zikisemwa Nairobi mitaani zilikuwa Sheng, KiKikuyu, Kikamba, Kijaluo, na Kiluhya (Lugha za kiLuhya abazo nilisikia sana kwa majirani hapo Kaloleni zilikuwa ni Kimaragoli, Kinyore, KiManyala, na zingine za kutoka Kakamega). Katika uwanja wa City Stadium, lugha ambazo nilisikia sana sikisemwa na mashabiki wa soka ni Kijaluo, Kiluhya, na Kiswahili.

Screen Shot 2025-12-02 at 8.02.33 PM.png

Ujirani

Hapo Shauri Moyo, ng’ambo ya mtaa wa Kaloleni, kuna vituo vya Shauri Moyo Baptist Church and Center na Shauri Moyo YMCA. Vituo hivyo vilichangia kwa wingi kwa vijana wa maeneo hayo kukuuza talanta za michezo mbalimbali, hasa basketball na indoor soccer. Dada yangu ambaye ninamfuata (Mercy Akura) alikuwa point guard wa timu ya basketball ya Kenya na Barclays Bank. Mwingine mchezaji hodari wa BB kutoka Kaloleni ni Jafred Amugune (Kenya National Team/Central Bank of Kenya). Amugune ni kaka wa aliyekuwa Chief Government Pathologist, Marehemu Dr. Alex Kirasi Olumbe) Wao walikuwa majirani wetu hapo Ololo.

MICHEZO MTAANI

Hapo katika uga wa Majimbo ulioko mtaa wa Kaloleni, kulikuwa na mashindano ya mpira, kila mwaka wakati wa likizo ya Aprili, ulio julikana kama “Majimbo Tournament.” Haya mashindano ya majimbo yalikuwa yanajumuisha majimbo ya mkoa wa Luo Nyanza (nadhani hii ndiyo ilikuwa asili ya jina la huo uga - Majimbo Field).

Majimbo haya yalikuwa kama Alego, Ugenya, Imbo, Sakwa, Uyoma, na mengine ya South Nyanza. Washiriki wa mashindano ya Majimbo walikuwa wakitoka katika sehemu zote za Nairobi, sio tu wakaazi wa Kaloleni.

Lugha ulizozisisikia zikisemwa Nairobi mitaani, shuleni, viwanjani, na kwingineko ulipokuwa mdogo. Nilipokuwa mdogo, lugha ambazo nilizisikia zikisemwa Nairobi mitaani zilikuwa Sheng, KiKikuyu, Kikamba, Kijaluo, na Kiluhya (Lugha za kiLuhya abazo nilisikia sana kwa majirani hapo Kaloleni zilikuwa ni Kimaragoli, Kinyore, KiManyala, na zingine za kutoka Kakamega). Katika uwanja wa City Stadium, lugha ambazo nilisikia sana sikisemwa na mashabiki wa soka ni Kijaluo, Kiluhya, na Kiswahili.

Screen Shot 2025-12-02 at 8.22.59 PM.png

Hizi timu mbili, Black Mamba Sports Club na Kaloleni Welfare Sports Club ziliweza kutoa wachezaji wengi sana ambao walicheza kwenye ligi kuu ya Kenya, baadhi yao wakiwa ndugu wangu watatu (Nick Akura, Peter “Pierre” Ochieng, na Atanas Otieno) ambao waliweza kuchezea timu ya Gor Mahia FC na KTM ya Thika). Mimi nilichezea timu ya Chuo Kikuu Cha Kenyatta - Hard Nuts FC.

Mama wangu alikuwa anafanya kazi katika Kliniki za City Council, kwa hivyo, lugha ambazo nilisikia zikisemwa sana na wafanyakazi ni Kikuyu na Kiswahili. Zahanati za City Council ambazo niliwahi kuenda kumsaidia mama wangu akifanya kazi zilikuwa Kaloleni, Punwani, Rhodes Avenue, Jericho, na Makadara. Idadi kubwa ya wafanyakazi wa City Council walizungumza lugha ya Kikuyu.

Lugha zilizotumika sana katika shule za msingi Nairobi, ni Kiswahili na Sheng tukiwa nje ya darasa, na Kingereza ndani ya darasa 1.Tajriba yako na lugha ya Sheng. Ulisema ndugu wako na wenzake walikuwa waasisi wa Sheng. Tafadhali elezea zaidi na utupe mifano mwafaka. Naamini kwamba ndugu wangu mkubwa na rika zake ambao walizaliwa kati ya miaka ya 1945 -1955 huko Eastlando ndio walikuwa waasisi wa sheng. Naamini kivyo kwa sababu wazazi wetu, wengi wao ambao walipigana katika vita vya pili vya dunia, hawakuzungumza sheng, lakini kizazi cha kaka yangu mkubwa kilizungumza sheng.

Screen Shot 2025-12-19 at 6.12.42 AM.png

​

Hapo Shauri Moyo, ng’ambo ya mtaa wa Kaloleni, kuna vituo vya Shauri Moyo Baptist Church and Center na Shauri Moyo YMCA. Vituo hivyo vilichangia kwa wingi kwa vijana wa maeneo hayo kukuuza talanta za michezo mbalimbali, hasa basketball na indoor soccer. Dada yangu ambaye ninamfuata (Mercy Akura) alikuwa point guard wa timu ya basketball ya Kenya na Barclays Bank. Mwingine mchezaji hodari wa BB kutoka Kaloleni ni Jafred Amugune (Kenya National Team/Central Bank of Kenya). Amugune ni kaka wa aliyekuwa Chief Government Pathologist, Marehemu Dr. Alex Kirasi Olumbe) Wao walikuwa majirani wetu hapo Ololo.

​

MICHEZO MTAANI

​

Mbali na michezo, kituo cha Baptist Center iliwapa vijana chumba au darasa la kufanya “Homework” wakati wa jioni kwa sababu nyumba nyingi hapo Eastlando hazikuwa na umeme. Baadhi ya wachezaji mashuhuri kutoka Kaloleni ni Nick Akura, Peter Pierre Ochieng, George “Vigo” Otieno, Jerry Imbo, Edward Kiiza, Neville Pudo, Joe Oyando, John Busolo, Lumumba Magunga, Jeff Fwaya, Jomo Opwande, na Mark Shida. Black Mamba Sports club pia ilikuwa na timu hodari sana ya Handball.

Vijana wa Black Mamba na Kaloleni Welfare walizungumza lugha ya Sheng kwa sababu walitoka katika jamii mbali mbali za Kenya na pia Uganda (kwa mfano Edward Kizza na nduguze ambo walikuwa wachezaji hodari wa kandanda).

Hapo katika uga wa Majimbo ulioko mtaa wa Kaloleni, kulikuwa na mashindano ya mpira, kila mwaka wakati wa likizo ya Aprili, ulio julikana kama “Majimbo Tournament.” Haya mashindano ya majimbo yalikuwa yanajumuisha majimbo ya mkoa wa Luo Nyanza (nadhani hii ndiyo ilikuwa asili ya jina la huo uga - Majimbo Field). Majimbo haya yalikuwa kama Alego, Ugenya, Imbo, Sakwa, Uyoma, na mengine ya South Nyanza. Washiriki wa mashindano ya Majimbo walikuwa wakitoka katika sehemu zote za Nairobi, sio tu wakaazi wa Kaloleni.

Lugha ulizozisisikia zikisemwa Nairobi mitaani, shuleni, viwanjani, na kwingineko ulipokuwa mdogo. Nilipokuwa mdogo, lugha ambazo nilizisikia zikisemwa Nairobi mitaani zilikuwa Sheng, KiKikuyu, Kikamba, Kijaluo, na Kiluhya (Lugha za kiLuhya abazo nilisikia sana kwa majirani hapo Kaloleni zilikuwa ni Kimaragoli, Kinyore, KiManyala, na zingine za kutoka Kakamega).

Katika uwanja wa City Stadium, lugha ambazo nilisikia sana sikisemwa na mashabiki wa soka ni Kijaluo, Kiluhya, na Kiswahili.

​

​

Screen Shot 2025-12-19 at 6.28.18 AM 1.png

Ndugu wangu mkubwa alizaliwa katika eneo la Nairobi South ambapo kulikuwa na makazi duni yasiyo rasmi (informat settlement) na kulelewa mitaa ya Bahati na Kaloleni. Kumbuka kwamba mtaa wa Kaloleni ulijengwa baada ya vita vya pili vya dunia (1945-1948). Kizazi changu ni cha kati ya 1956 -1966. Mengi ya maneno haya ya Sheng yalibadilika (evolved) kadri muda ulivyosonga mbele

​

1.Kulikuwa na wasemaji lugha kutoka mataifa mengine ya Afrika au kwingineko? Hapo Kaloleni, najua familia mbili tu, moja kutoka Uganda and nyingine Tanzania.

​

1.Ulinieleza jinsi sera za serikali ya kikoloni zilivyoathiri hali ya lugha katika mitaa mbalimbali jijini Nairobi. Kwa mfano, eti jinsi makabila yalivyotenganishwa au wasemaji wa

lugha tofauti walivyotenganishwa. Hebu elezea zaidi uliyoyashuhudia. Eh ndiyo. Babangu alinieleza kwamba hali ya hatari ilipotangazwa na serikali ya kikoloni Okotba

1952 kwa sababu ya vita vya Mau Mau, wafrika wa jamii ya Kikuyu ambao waliishi mitaa mbalimbali ya Nairobi walihamishwa na kupelekwa katika mtaa wa Bahati. Hi ni kwa sababu wengi wao walishukiwa kuwa wanachama wa Mau Mau! Wakati huo, wazazi wangu walikuwa wakiishi mtaa wa Bahati. Wao walitengewa nyumba katika mtaa wa Kaloleni, ambayo ilikusudiwa pia kuwa makazi ya familia. Mtaa wa Kaloleni ilijengwa miaka ya 1946 - 1948. Kipaumbele (priority) kilipewa wafrika waliohudumu katika jeshi la waingereza kule Burma na Abyssinia wakati wa vita vya pili vya dunia. Hii ndiyo sababu kubwa ya wakaazi wa Bahati kuwa ya jamii ya wakikuyu na Kaloleni na Ziwani ikawa na idadi kubwa ya wakaazi kuwa wajaluo na waluhya.

​

Mtaa wa Kaloleni ulikuwa wa “kifahari” kuliko mitaa mengine ya waafrika kwa sababu design yake ilikuwa ya aina ya bustani (garden city) iliokuwa na maeneo mengi ya wazi. kila nyumba Kaloleni ilikuwa pia na vyumba viwilii au vitatu (one or two bedrooms) pamoja na jikoni ndogo. Nyumba hizo, hata hivyo, havikuwa na vyoo vya ndani. (tazama “kandoya” kwa lugha ya Sheng)

Mtaa huu pia ulkuwa na shule ya msingi (St. Johns primary), kituo cha afya (Kaloleni dispensary), zahanati (Kaloleni clinic), na ukumbi wa kijamii (Kaloleni Social Hal) ambao ulikuwa wa pili kwa ukubwa ukilingnisha na City Hall. Ukimbii huu ulitumika sana na wanasiasa maarufu waafrica kama vile Jomo Kenyatta na Tom Mboya. Kaloleni pia ilikuwa na “shopping center” ambacho pia kilikuwa na baa (tatu).

​

1. Mitaaa mipya kama Buruburu na Umoja. Ilijengwa lini? Iliathiri kwa njia gani eneo la Eastando?  Ni watu gani waliokuwa wa kwanza kuishi humo?

aa mipya kama Buruburu na Umoja. Ilijengwa lini? Iliathiri kwa njia gani eneo la Eastando?  Ni watu gani waliokuwa wa kwanza kuishi humo?

New Pumwani/California replacing some of the old Pumwani/Majengo slums Kimathi Estate (between Bahati and Eastleigh Section 3) Biafra Estate (between Shauri Moyo and Eastleigh/New Pumwani/California) Buru Buru Phase 1: 1973 - 1975 Buru Buru Phase 5: 1984 Umoja

​

1.Ukiwa na picha za kitambo hicho haswa zinazoonyesha maeneo tofauti uliyotaja zitafaa sana. Picha:Kaloleni Estate (circa 1982)

1.Ikiwa kuna mengineyo yanayohusu lugha ambayo sikuyashughulikia, tafadhali ongezea. Hamna nyongeza mbaya ila… Ni dhahiri kwamba sera ya serikali ya kikoloni iliyoruhusu wafrika wanaume kuleta familia zao mjini ndiyo ilichangia pakubwa kwa kunawiri kwa lugha ya Sheng. Kabla ya mwaka wa 1940, sera ya kikoloni ilikuwa kwamba wafrika waliishi mijini kwa mda mfupi tu (Harris & Hay, 2007). Waafrika wanaume amboa wilkuwa wafanyakazi waliishi kwenye mitaa ya ma “bachelor” kama vile Makongeni, Muthurwa, Shauri Moyo, na Pumwani Baada ya 1940, serikali ya wakoloni ilianza kujenga nyumba za familia kama vile Ziwani na Kaloleni. Hao watoto wa wafanyakazi waafrika ambao sasa walijikuta wakiishi mijini na kutangamana na watoto wenzao kutoka sehemu nyingine za nchi hawakuwa na budi ila kubuni lugha yao ya mtaa!

Sina hakika hasa ni nani aliyekuja na hilo jina “Sheng!! Nillisikia kwa mara ya kwanza kutoka kwa mwanahabari moja wa gazeti.

​

Hizi timu mbili, Black Mamba Sports Club na Kaloleni Welfare Sports Club ziliweza kutoa wachezaji wengi sana ambao walicheza kwenye ligi kuu ya Kenya, baadhi yao wakiwa ndugu wangu watatu (Nick Akura, Peter “Pierre” Ochieng, na Atanas Otieno) ambao waliweza kuchezea timu ya Gor Mahia FC na KTM ya Thika). Mimi nilichezea timu ya Chuo Kikuu Cha Kenyatta - Hard Nuts FC.

​

Mama wangu alikuwa anafanya kazi katika Kliniki za City Council, kwa hivyo, lugha ambazo nilisikia zikisemwa sana na wafanyakazi ni Kikuyu na Kiswahili. Zahanati za City Council ambazo niliwahi kuenda kumsaidia mama wangu akifanya kazi zilikuwa Kaloleni, Punwani, Rhodes Avenue, Jericho, na Makadara. Idadi kubwa ya wafanyakazi wa City Council walizungumza lugha ya Kikuyu.

Lugha zilizotumika sana katika shule za msingi Nairobi, ni Kiswahili na Sheng tukiwa nje ya darasa, na Kingereza ndani ya darasa 1.Tajriba yako na lugha ya Sheng. Ulisema ndugu wako na wenzake walikuwa waasisi wa Sheng. Tafadhali elezea zaidi na utupe mifano mwafaka. Naamini kwamba ndugu wangu mkubwa na rika zake ambao walizaliwa kati ya miaka ya 1945 -1955 huko Eastlando ndio walikuwa waasisi wa sheng. Naamini kivyo kwa sababu wazazi wetu, wengi wao ambao walipigana katika vita vya pili vya dunia, hawakuzungumza sheng, lakini kizazi cha kaka yangu mkubwa kilizungumza sheng.

​

​

​

​

​

​

Maisha na Lugha Nairobi: Tajriba Ya Dkt. Okong'o Akura.

Nilizaliwa na kulelewa katika mtaa wa Kaloleni ulioko hapo Jogoo Road, karibu na soko la Burma. Kaloleni, kwa lugha ya Sheng ni “Ololo”.  Ukitazama kwenye ramani, utaona kwamba mtaa wa Kaloleni umezingirwa na mtaa wa Shauri Moyo (Sheng = Shauri) ulioko kaskazini mwa Kaloleni. Mashariki na kusini mashariki mwa Kaloleni ni Mtaa wa Makongeni (Sheng = Okongo) ambao ni ya wafanyakazi wa Shirika la Reli (East African Railways and Harbours/ Kenya Railways). Kusini magharibi ni eneo la viwanda lijulikanalo kama Industrial Area (Inda). Magharibi mwa Kaloleni ni mitaa ya Railway, Muthurwa, na Landi Mawe. Wengi wa wakazi wa Landi Mawe walikuwa ni Wahindi ambao walikuwa wafanyakazi wa reli. Utaona kwamba katikati ya jiji la Nairobi (Kenyatta International Conference and Convention Center) ni umbali wa takriban kilomita tatu tu kutoka Kaloleni. 

Shule nilizohudhuria 

​

Nilihudhuria shule ya msingi ijulikanayo kama St. John Primary School papo hapo Kaloleni. Shule hii ilikuwa chini ya Baraza za Mji wa Nairobi (City Council of Nairobi) lakini ilidhaminiwa na Kanisa Katoliki, kama vile shule zingine za msingi za Nairobi kama St. Peters Clavers, St. Anne, Our Lady of Mercy Shauri Moyo, St. Paul’s, St. Patrick’s, n.k. 

​

Kisha, nikahudhuria shule ya upili ya Dr. Ribeiro Parklands High School katika mtaa wa Parklands. Tulikuwa tukitembea kwa miguu kuenda shule Parklands kila siku, takriban Kilomita 7 kutoka Kaloleni. Wengi wa wakazi wa mtaa wa Parklands walikuwa ni Wahindi. Masomo ya “A’ Levels, nilienda Kanunga High School ilioko County ya Kiambu.

​

​

Screen Shot 2025-10-28 at 11.21.06 PM.png
Screen Shot 2025-10-28 at 10.07.51 PM.png
bottom of page